Mawasiliano ya mtandao yamejikita katika modeli ya kuhifadhi na kutuma ambayo inaweza ikaeleweka katika mfumo wa zamani kwenda kwenye barua ya posta: Taarifa husafirishwa katika vitalu vinavyoitwa datagram au pakiti.
Kila pakiti inahusisha chanzo cha anwani za IP (kwa mtumaji) na anwani ya IP ya eneo kusudiwa (mpokeaji), kama barua ya awali zinazobeba anwani ya posta ya mtumiaji na mpokeaji.
Kutoka kwa mpokeaji hadi kwa mtumaji inahusisha hope nyingi za routers, ambapo kila router inakagua anwani ya IP ya eneo husika na kutuma pakiti karibu na eneo kusudiwa.
Hivyo, kila router kati ya mtumaji na mpokeaji anagundua kuwa mtumaji anawasiliana na mpokeaji.
Haswa, ISP wako wa ndani wako na nafasi ya kutengeneza maelezo yaliyokamilika katika matumizi yako ya mtandao .
Sambamba na hayo, kila seva katika mtandao ambayo inaweza kuona pakiti yeyote inaweza kupata tabia yako.
Lengo la Tor ni kuimarisha faragha yako kwa kutuma upekuzi wako kupitia mfululizo wa proxy.
Mawasiliano yako yamesimbwa kwa safu nyingi na kupitishwa na hop kupitia mtandao wa Tor kwa mpokeaji wa mwisho.
Taarifa zaidi kuhusu mchakato zinaweza kupatikana kupitia kielelezo hiki] .
Zingatia ISP wako wote wa ndani wanaweza kuona sasa unawasiliana na node za Tor.
Sambamba na hilo, seva katika mtandao zinaona kwamba umewasiliana na node za Tor.
Kwa ujumla, Tor imelenga kutatua matatizo matatu ya faragha:
Kwanza, Tor huzuia tovuti na huduma nyingine kujua eneo lako, ambalo wanaweza kutumia kutengeneza kanzidata kuhusu mazoea na vivutio vyako.
Kupitia Tor, muunganiko wa mtandao wako haukupeleki mbali kiotomatiki-- sasa unaweza kuchagua, kwa kila muunganiko, ni taarifa ngapi kufichua.
Pili, Tor huzuia watu kuangalia upekuzi wako mtandaoni (kama vile ISP wako au mtu yeyote aliyepata wifi au router ya nyumbani kwako) from learning taarifa zipi unazipekua na wapi umezipekua.
Pia inawasimamisha kutoka kuamua vitu unavyoruhusiwa kujifunza na kuchapisha -- kama unaweza kupata kila upande wa mtandao wa Tor, unaweza ukaifikia kila tovuti katika mtandao.
Tatu, Tor huelekeza muunganisho wako kupitia zaidi ya Tor relay moja, hivyo kakuna relay moja inaweza kuona kile unachopekua.
Kwa sababu relay hizi zinaendeshwa na watu au taasisi tofauti, ulinzi wa watoa huduma za usambazaji wa seva ni imara zaidi ya awali hop moja ya proxy] mbinu ya .
Zingatia, japokuwa, kuna mazingira ambapo Tor hushindwa kutatua matatizo haya ya faragha: tazama ingizo hapa chinimashambulizi yaliyobaki] .