Kubwa zaidi, ndiyo sababu tulitekeleza sera ya kuondoka.
Kila Tor relay ina sera ya kutoka ambayo inabainisha aina gani ya muunganiko wa nje unaruhusiwa au unakataliwa kutoka kwenye hiyo relay.
Sera za kutoka zinaenezwa kwa watumiaji wa Tor kupitia saraka, hivyo mtumiaji atapaswa kuepuka kuchagua relays za kutoka kiotomatiki ambazo zitakataa kutoka katika lengo lao.
Kwa njia hii kila relay inaamua huduma, mmiliki, na mtandao inaoutaka ili kuruhusu muunganiko, kulingana na uwezekano wa unyanyasaji na hali yake mwenyewe.
Soma Ingizo la msaada kwenye masuala unayoweza kukutana nayo] ikiwa unatumia sera za kutoka za kawaida, na pia soma Mike Perry's vidokezo vya kutumia exit node kwa unyanyasaji kidogo.
Sera za kawaida za kutoka zinaruhusu kufikiwa kwa huduma nyingi zinazojulikana (mfano kuvinjari tovuti), lakini zinazuia baadhi kutokana na uwezekano wa matumizi mabaya (kwa mfano barua pepe) na zingine kwani mtandao wa Tor hauwezi kushughulikia mzigo (kwa mfano sakiti za kusambaza mafaili kwa njia ya kawaida).
Unaweza kubadilisha sera yako ya kutoka kwa kuhariri faili lako la torrc.
Ikiwa unataka kuepuka zaidi kukiwa hakuna uwezekano wowote wa unyanyasaji, pangilia iwe "reject *:*".
Mpangilio huu unamaanisha kuwa relay yako itatumika kwa relaying ya kusafirisha data ndani ya mtandao wa Tor, lakini sio kwa mawasiliano ya tovuti za nje au kwa huduma zingine.
Ikiwa hutaruhusu mawasiliano yeyote ya kutoka, hakikisha azimo la jina linafanya kazi (hii ni, kompyuta yako inaweza kutatua anwani za mtandao kwa usahihi).
Kama kuna vyanzo vyovyote ambao komputa haiwezi kuvifikia (kwa mfano, upo nyuma ya programu za ulinzi zilizozuiliwa au maudhui yaliyo chujwa), tafadhali wazikatae katikasera yako ya kutoka vinginevyo watumiaji wa Tor wataathiriwa pia.